Psalms 150

Msifuni Bwana Kwa Ukuu Wake

1 aMsifuni Bwana.

Msifuni Mungu katika patakatifu pake,
msifuni katika mbingu zake kuu.
2 bMsifuni kwa matendo yake makuu,
msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.
3 cMsifuni kwa mvumo wa tarumbeta,
msifuni kwa kinubi na zeze,
4 dmsifuni kwa matari na kucheza,
msifuni kwa kinanda cha nyuzi na filimbi,
5 emsifuni kwa matoazi yaliayo,
msifuni kwa matoazi yavumayo sana.

6 fKila chenye pumzi na kimsifu Bwana.

Msifuni Bwana!
Copyright information for SwhNEN